Mahakama kuu nchini Malawi
imesema kuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na makamishna wa tume hiyo
wanakabiliwa na mashitaka ya kudharau amri za mahakama.
Jaji Healey Potani wa mahakama kuu ya Blantyre
amesema kuwa Jaji mwenzie Mack Mbendera na tume yake yote wamedharau
mahakama kwa kuendelea na mipango ya kurudia kuhesabu kura ilhali
Mahakama kuu kupitia kesi iliyowasilishwa na chama cha DPP iliiamuru
tume hiyo kutangaza matokeo yote na kama kuna malalamiko yatafuata
baadae.'Tume kufikishwa Kortini'
Hali hii inatazamiwa kuongeza utata katika suala zima la kupatikana hatma ya uchaguzi huo, ukizingatia kuwa Jumatatu usiku mwenyekiti wa tume hiyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa, huenda mchakato huo ukachukua hadi siku 30 zijazo.
Hata hivyo Jaji Mbendera amesema tume yake inasubiri uamuzi wa Mahakama kuu ya Malawi iiongezee muda zaidi wa kuhesabu na kutoa matokeo, kwani muda wa sasa kisheria ni siku nane tu ambazo ni kama zimekwisha.
Wakati mivutano ikiendelea nao viongozi wa vyama mbalimbali nchini hapa wanawataka wafuasi wao na wananchi kwa ujumla kutulia na kusubiri tume ifanye kazi yake kwa mujibu wa sheria.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa kila kinachojiri kutoka huko Malawi
0 comments:
Post a Comment