Malawi ni miongoni mwa nchi
zinazozalisha tumbaku kwa wingi duniani. Uchumi wa nchi hiyo iliyoko
kusini mwa bara la Afrika unategemea kilimo cha zao hilo kwa asilimia
75.
Ikiwa leo ni siku ya kutovuta tumbaku duniani,kila
unapopita mitaani kwenye miji mikubwa ya Lilongwe na Blantyre na hata
maeneo ya vijijini hakuna tofauti.
Malawi haijaathirika kwa lolote kwenye kilimo cha zao hili isipokuwa tu misukosuko ya kawaida
'Mhimili wa uchumi wa nchi'
Tumbaku ndiyo dhahabu ya Malawi, wenyewe wanasema bila tumbaku hakuna maisha
Kijana mmoja amezungumza akasema yeye havuti sigara na anafahamu vizuri madhara ya kuvuta sigara, lakini wao kama nchi hawawezi kuacha kulima tumbaku kwani ndiyo msingi wa uchumi wa Malawi, na hawana bidhaa nyingine mbadala ya kufidia kilimo cha tumbaku itakapobidi kuacha kulima zao hilo.
Wamalawi walioko mashambani na hata mijini kwa umoja wao bila kujali wasomi ama mbumbumbu, wana kitetea kilimo cha tumbaku kwa nguvu zote.
Mkulima wa zao hilo Amon Ndewere ambaye anamiliki shamba la ekari 40 anasema kelele za ulimwengu kupiga vita kilimo cha tumbaku kwao hazina tija kabisa wanachoangalia ni jinsi gani wanunuzi na serikali watawaboreshea maisha yao bila kuwanyonya.
'Tumbaku inauzwa kwa mnada
Huko wanakutana na wanunuzi ambao ni makampuni makubwa ya kimataifa kama Alliance One, Japan Tobacco, Malawi Leaf na mengine.
Afisa mtendaji Mkuu wa Tume ya udhibiti wa tumbaku nchini Malawi Bruce Muthali, Anasema kazi yao ni kusimamia sera ya zao hilo listawi kwa manufaa ya nchi na watu wake.
'Tumbaku ya kipekee duniani'
Na kwa hakika nchi hii haijaathirika kwa lolote kwenye kilimo cha zao hili isipokuwa tu misukosuko ya kawaida ya kupanda na kushuka kwa bei ya tumbaku kwenye soko la dunia.
Inaelezwa kuwa Malawi kuna wavutaji wengi wa sigara, lakini serikali ilifunga kiwanda chake cha kutengeneza sigara zaidi ya miaka 15 iliyopita,na sasa kuna kiwanda kidogo tu kimoja, sigara zote zinazopatikana nchini humo zinatoka nchi jirani na hasa Zambia na Msumbiji huku Tanzania na Afrika Kusini zikichangia ongezeko kidogo sana.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kusoma makala mbalimbali ambazo zinamantiki na kusadifu maisha halisi ya mwanadamu na changamoto mbalimbali katika maisha.
0 comments:
Post a Comment