Moto mkubwa ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo yenye uzito wa tani 998 iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea ndani ya maji baada ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na majanga ya moto.
Watu saba wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne wakiuguza majeraha ya moto kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo kapteni wa meli hiyo amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado unaendelea.
Afisa usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti kuwa wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli wakati mlipuko unatoke.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata taarifa mbalimbali zinazojiri sehemu mbalimbali katika kila pande ya dunia.
0 comments:
Post a Comment