Kampuni
ya magari ya Lamborghini imetengeneza gari hili maalum Huracan LP 610-4
kwa ajili ya polisi wa Italia. Magari haya yatachukua nafasi ya magari
ya zamani aina ya Lamborghini
Gallardo ambayo tayari yanatumika
kupiga doria, limeripoti shirika la habari la Italia, ANSA. Kasi yake
ni kilomita 325 kwa saa. Lina kila aina ya teknolojia ya kisasa pamoja
na kamera za video kupiga picha wakati ikifukuza wahalifu.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata habari na stori mbalimbali ambazo haujazisikia na hautazisikia sehemu nyingine ambazo ni muhimu na zinafurahisha.
0 comments:
Post a Comment