Thursday, 29 May 2014
Kenya yakamata shehena ya mti wa Rosewood wenye thamani kubwa
Kenya imekamata shehena ya mti mwekundu -rosewood- yenye thamani ya dola milioni 6.6. Kwa mujibu wa maafisa wa Kenya, magogo hayo adimu yamekamatwa katika bandani ya Mombasa yakisafirishwa kutoka Madagascar kwenda Hong Kong. Wanamazingira wanasema ukataji miti haramu umeongezeka kwa kasi nchini Madagascar tangu mapinduzi nchini humo mwaka 2009. Miti hiyo ya mbao hutumika kutengenezea samani (fanicha) zenye thamani kubwa.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari zinazovutia na zenye mantiki ambazo hautakiwi kuzikosa.Jukuma letu sisi ni kukuhabarisha pale tunapopata habari yoyote.
0 comments:
Post a Comment