Kocha mpya wa Manchester United ,
Louis van Gaal anapania kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza katika mwaka wake wa kwanza tangu achukue usukani Old
Trafford.
Van Gaal anajivunia rekodi ya kutwaa taji la
ligi katika mwaka wake wa kwanza alipoiongoza Barcelona kutwaa taji la
Uhispania msimu wa 1997-98 na kisha akarejelea tena ushindi akiiongoza
Bayern Munich ya Ujerumani mwaka wa 2009-10.Iwapo atafaulu Van Gaal atajiunga na makocha wengine watatu Jose Mourinho na Carlo Ancelotti wa Chelsea na Manuel Pellegrini wa Manchester City.
Akizungumza katika mahojiano na runinga ya kitaifa huko Uholanzi, RTL van Gaal mwenye umri wa miaka 62 alisema itakuwa bora iwapo Manchester Utd itarejea kileleni Uingereza.
Van Gaal, ambaye ameasaini mkataba wa miaka mitatu amewahi kushinda mataji saba tofauti akiwa na vilabu vinne tofauti - Ajax, Barcelona, AZ Alkmaar na Bayern Munich.
United ilimaliza katika nafasi ya 7 katika msimu uliokamilika wa 2013-14 na ikashindwa kufuzu kwa michuano ya bara ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na michezo kutoka katika kila pande ya dunia kwa wakati muafaka bila kuchelewa
0 comments:
Post a Comment