Facebook

Friday, 16 May 2014

Aliyefichua kanda ya Jay-Z akishambuliwa afutwa kazi


Solange alimshambulia Jay Z katika lift walipokuwa wanatoka tamashani
Mfanyakazi aliyefichua kanda inayoonyesha mwanamuziki Jay Z akishambuliwa na shemeji yake , amefutwa kazi.
Kamera ya lifti ilinasa vurumai kati ya Jay Z na shemeji yake Solange Knowles aliyeonekana kuwa na hasira mno huku akimshambulia Jay Z , ingawa haijulikani kilichosababisha vita hivyo kwenye lifti.
Kanda hiyo ya video ambayo ilitolewa kwanza kwenye tovuti ya udaku kuhusu watu maarufu TMZ, ilimwonyesha dadake Beyonce akimpiga Jay Z baada ya tamsha la Met mjini Los Angeles, iliyofanyika mwezi Mei tarehe 5.
Baada ya ugomvi mkali baina yao, mlinzi aliingilia kati. Hata hivyo kanda hiyo haikuwa na sauti.
Hoteli hiyo inayojulikana kama ‘The Standard ilisema kuwa ilishtushwa sana na kufichuliwa kwa matukio ya Lifti na ikamtaja mfanyakazi huyo aliyehusika katika ufichuzi huo.
Mfanyikazi huyo alifutwa kazi kwa kosa la kuvunja sheria za usalama kwa kufichua video za CCTV, ambazo ni za siri.
Hoteli hiyo iliongeza kuwa ingetoa habari zingine zote za ziada kwa idara ya kupambana na wakiukaji wa sheria.
Waakilishi wa Jay Z, Beyonce na Solange hawajasema lolote kuhusiana na tukio hilo.

Related Posts:

  • Wema mama Kijacho,anasa mimba ya Diamond.! ‘Beautiful  Onyinye’  na  kipenzi  cha  Diamond, Wema  Sepetu  sasa  ni  mjamzito. Baada  ya  misukosuko  ya  muda  mrefu  ikiwemo  kuporwa … Read More
  • Rapper Eve aolewa   Msanii maarufu wa miondoko ya kufokafoka - rap- nchini Marekani Eve, ameoana rasmi na mchumba wake Maximillion Cooper, katika mji wa Ibiza nchini Spain. Cooper ni muasisi wa mashindano ya mbio za magari za Gumb… Read More
  • Penny afunguka baada ya kupona. MTANGAZAJI wa maarufu wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa ugonjwa uliompiga juzikati ulikuwa ‘serious’ kiasi cha kuona ni Mungu tu amemwokoa. Akichezesha taya na paparazi wetu, Penny al… Read More
  • Alichokisema Wema Sepetu Kuhusu Penzi lake na Diamond. Wema Sepetu amesema uhusiano wake na Diamond Platnumz kwa sasa ni imara kwa kuwa wamepitia mambo mengi pamoja yaliyowafunza mengi. Akiongea hivi karibuni akiwa jijini Durban, Afrika Kusini alikoenda kuhudhuria t… Read More
  • Birthday ya Vicenti Kigosi "ray", Johari ampa salamu tata !! Jana mwigizaji maarufu nchini Vicent kigosi - Ray amesherehekea siku yake ya kuzaliwa huku akipata salamu mbalimbali za pongezi toka kwa mastaa mbalimbali nchini. Moja ya watu wa kwanza kw… Read More

0 comments:

Post a Comment