Wednesday, 7 May 2014
Arsene Wenger Asingedumu Hispania Kama Angekuwa Kocha kwenye Ligi Hiyo
KOCHA Mkuu wa West Brom, Pepe Mel amesema kocha Arsene Wenger kushindwa kutwaa mataji kwa muda mrefu huku akiwa na kikosi imara kama cha Arsenal ana bahati sana kwa sababu kazi yake anafanya England na kama angekuwa Hispania angefukuzwa kazi siku nyingi.
Arsenal haijatwaa taji lolote la maana tangu mwaka 2005 ilipotwaa Kombe la FA na msimu huu wanaweza kumaliza ukame huo kama wataifunga Hull City kwenye fainali ya Kombe la FA itakayofanyika Mei 17 uwanjani Wembley, London.
Mel anasapoti falsafa za kocha huyo Mfaransa, lakini anashangaa ni vipi anakinoa kikosi chenye wachezaji makini kama cha Arsenal na kushindwa kunyakua mataji.
Wakati Gerardo Martino akijiandaa kuondoka Barcelona mwisho wa msimu, Wenger anapewa nafasi ya kurithi mikoba, lakini Mel anamtaka aendelee tu kubaki England kwa sababu kama atakwenda Hispania hatadumu kwa muda mrefu kwa kuwa na timu isiyotwaa mataji.
“Sidhani kama Arsene angeweza kudumu na kibarua chake nchini Hispania,” alisema Mel, 51.
“Carlo Ancelotti ni mfano mzuri pale Real Madrid. Miezi mitatu iliyopita alikuwa kwenye presha kubwa sana kabla ya sasa kupoa kwa sababu ameifikisha timu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hispania kocha anaishi kutokana na matokeo.”
Related Posts:
Liverpool yazidi kupaa Ligi Kuu Uingereza. Majogoo wa Liverpool leo wameonesha makucha yao katika mchezo wa ligi kuu ya England baada ya kuichapa timu ngumu ya Southampton mabao 2-0. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Philippe Coutinho dakika ya 3 na Raheem Sterli… Read More
Yanga yazidi kutakata Mbeya, Simba Hoi ShinyangaTimu ya Yanga imejibebea point nyingine tatu katika mkoa wa Mbeya baada ya leo kuichapa timu ngumu ya Mbeya City jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara. Mabao ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva dakik… Read More
BantuTz MAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO FEBRUARI 23 BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa ka… Read More
Mayweather kuzichapa na Pacquiao Mwanamasumbwi raia wa Marekani Floyd Mayweather Junior ametangaza kuwa pigano lililosubiriwa kwa siku nyingi na mwanamasumbwi raia wa ufilipino Manny Pacquiao litafanyika mjini Las Vegas tarehe mbili mwezi Mei mwaka huu Pamb… Read More
Sony kuuanza utengenezaji wa filamu na vipindi vya burudani Kampuni ya Sony imetangaza wiki hii kwamba itajiondoa katika michezo ya kielektroniki katika idara zake za sauti na video.Badala yake inapanga kuangazia maeneo matatu ikiwemo idara yake ya filamu,burudani,michezo yake ya Play… Read More
0 comments:
Post a Comment