Sunday, 4 May 2014
Dr.Kigwangala autolea udenda Urais 2015
MBUNGE wa jimbo la Nzega Mkoani Tabora kupitia CCM, Hamis Kigwangala, ametanabaisha kuwa anatafakari kama anaweza kugombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha mapinduzi CCM.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua fununu zilizo enea kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiibua mijadala mara kwa mara inayomshawishi kugombea Urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala amesema anatafakari jambo hilo zito na kuongeza kuwa muda utakapofika atayazingatia maoni ya wananchi.
Akizungumzia maelezo kwamba haoni kama ni hatari kwake kutangazwa mapema kwamba anataka kuwa kugombea Urais ni kujipunguzia sifa katika chama chake, Dk. Kigwangala alisema yeye hajatangaza kama anataka Urais na wala hajamtuma mtu kuanza kumfanyia kampeni, kwani watanzania wanaongozwa na katiba yenye Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hivyo hayo ni mawazo yao na wana haki ya kufanya hivyo na yeye binafsi hawezi kuwapinga.
Hivi karibuni kumeibuka mijadala mizito kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wanaharakati kutengeneza vuguvugu la kumshawishi Dk. Kigwangala kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ifikapo mwaka 2015.
Mijadala hiyo mizito imeanzishwa katika mitandao ya Internet na simu za mkononi walio ipachika jina "Citizens for Kigwangala" ambapo katika mijadala hiyo wamekuwa wakishawishiana na kumwagia sifa Dk Kigwangala kwamba ndiye kiongozi pekee anayefaa kuwakilisha chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya vijana wamekuwa wakijadili kuwa Dk Kigwangala ndiye anayeweza kuleta upinzani wa kweli kwa vyama vya upinzani, wakijenga hoja kuwa amekuwa na misimamo na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha ndani ya vikao vya bunge.
Dk Kigwangala ni mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, mwenye taaluma ya udaktari wa tiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.
Related Posts:
Madereva Wagomea na Kukisusa Kituo Kipya cha Daladala Ubungo Mwenge Wamiliki na madereva wanayofanya safari zake kati ya Ubungo na Mwenge jijini Dar leo wamegomea amri ya kutumia kituo kipya walichoamriwa na serikali kukitumia kilichopo nyuma ya jengo la Mawasiliano Tower, Ubungo jij… Read More
Umeipata hii, ‘Nabii wa dengue’ aibuka Dar, ataka kumwona JK Serikali imetenga zaidi ya Sh700 milioni kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya Dengue ambayo imeendelea kushika kasi huku wengine wakipoteza maisha. Dar es Salaam. Wakati homa ya dengue ikizidi kusambaa … Read More
Bosi wa EWURA Akutwa Amefariki Hotelini Meneja Biashara wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) amekutwa amekufa hotelini katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitoka Dodoma ambako alihojiwa na… Read More
Homa ya Dengue Yaibua Tafrani Jijini DSM TAARIFA isiyo sahihi ya maambukizi ya homa ya dengue inayoenezwa na mbu aina ya aedes, imesababisha baadhi ya madereva teksi jijini Dar es Salaam, kujilinda kwa kuvaa glovu za mikononi, soksi ndefu miguuni na… Read More
Afia Kaburini Baada ya Kunaswa na Kitu Akijaribu Kufukua ili Aibe Fuvu Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti habari ya mtu mmoja aliyekutwa amefia kaburini kwamba alikubwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo… Read More
0 comments:
Post a Comment