Sunday, 4 May 2014
Je unaijua taarifa iliyotoka kuhusiana na ndege iliyopotea ya Malaysia....???
Toka March 8 2014 mpaka leo ikiwa ni May, ndege ya Malaysia iliyokua imebeba zaidi ya watu 200 haijulikani ilipo baada ya kupotea ikiwa inatokea Malaysia kwenda Beijing China.
Kwa siku zote hizo toka imepotea ndugu wa abiria wa ndege hiyo wamekua wakishinda kwenye hoteli ambazo pia zimekua zikitumiwa na shirika hilo la Malaysia kukusanyika na kutoa taarifa kuhusu kinachoendelea kwenye kuitafuta ndege hiyo.
May 1 2014 taarifa zimeanza kusambaa kwamba ndugu hao sasa wamepewa maagizo waondoke kutoka kwenye hoteli zote walizofikia Beijing na Kuala Lumpar na kurudi nyumbani kwao ambapo taarifa za chochote kitakachotokea watazipata wakiwa hukohuko majumbani.
Hii iliwafanya ndugu kadhaa kuangua tena vilio na kupiga mayowe baada ya kujua kwamba taarifa ya shirika hilo la ndege inamaanisha haitakuwepo tena ile mikusanyiko ya kila siku kwenye chumba cha mikutano kwa ndugu hao kupewa taarifa za kinachoendelea kwenye zoezi la utafutaji wa ndege hiyo.
Kwenye hoteli ya Lido Beijing ambako kampuni hiyo ya ndege imekua ikiwalipia ndugu hao wa abiria toka ndege ipotee, kulikua na watu wanaozidi 500 ambao wote ni ndugu wa abiria waliopotea.
Hata hivyo kampuni hii ya ndege itaanza kutoa malipo ya pesa kwa ndugu hao siku za karibuni ambapo japo haijasema itatoa kiasi gani, sheria inasema ndugu wanaweza kulipwa kuanzia dola za kimarekani laki moja na nusu mpaka laki moja na elfu 75.
Ripoti mpya iliyotoka inasema maafisa hawakua wamegundua kupotea kwa ndege hiyo mpaka dakika 17 baadae na walichelewa kwa dakika 240 kuanza kuitafuta ndege hiyo baada ya kupotea kwenye radar.
Related Posts:
Hivi ndivyo ambavyo wapishi wa chakula waliwaua wapiganaji wa IS Kumekuwa na mbinu mbalimbali zinazotumiwa na Vikosi vya Serikali ya Syria kupambana na wapiganaji wa IS ambazo bado hazijafanikiwa sana kutokana na changamoto mbalimbali. Wapiganaji wa Dola ya Kiislamu Syri… Read More
Viongozi wa China na Japan wakutana kuzimaliza tofauti zao. Rais wa Uchina, Xi Jinping na waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe wamefanya mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu wote washike madaraka. Mkutano wao unaonekana kama hatua ya ufanisis ya juhudi za kutatua taharuki iliyokuwepo ka… Read More
Papa ayaasa mataifa 20 tajiri duniani kuyakumbuka na kuyasaidia mataifa masikini.Papa Francis ametaka viongozi duniani wanaoshiriki mkutano wa G20 mjini Brisbane kuwafikiria watu masikini ulimwenguni. Amewataka Viongozi hao kupata ufumbuzi wa kuimarisha hali ya maisha ya watu walio masikini. Viongozi wa n… Read More
Wawili wanusurika kifo katika lile jengo jipya la World Trade Centre-Marekani.Wasafisha madirisha wawili mjini New York wanabahati ya kipekee kuepuka kifo baada ya jukwaa walilolitumia kusimama kuvunjika,na kuwaacha wakining'nia ghorofa ya sitini na tisa juu ya mji wa Manhattan ya chini. Wanaume hao wa… Read More
Unafahamu kwamba CNN walilipoti Obama kauwawa ? Ilishtua wengi na kuzua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii baada ya shirika la utangazaji Marekani CNN kuripoti kuuawa kwa Rais Obama. Makosa ya kiuandishi yalifanyika ambapo mtayarishaji wa video aliandika neno … Read More
0 comments:
Post a Comment