Mwanaume mmoja Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani
kuelekea Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita
Mombasa na baadae kwa ndege mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua ameziingiza
katika njia ya haja kubwa.
Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema mshukiwa
alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na baadae akatoa
tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa Mahakamani.
Mwezi March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo
walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75
za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Wanawake watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa kosa
la kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia
Namanga na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong.
Kuanzia March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano
wamekamatwa kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za
kusafirisha dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.
Related Posts:
Ashtakiwa kwa kuzinyofoa nyeti za mumewake kisa wivu na ugomvi wa kimapenzi..........
Jeshi la polisi mkoa wa Pwani
linamshikilia Husna Iddi Kisoma (19) , mkazi wa Kisemvule Mkuranga mkoa
wa Pwani kwa tuhuma za kumuua mumewe Jumane Mwalami (21) baada ya
kumvuta sehemu za siri na kuzi… Read More
Inasikitisha sana:Trafiki kafa ghafla akiwa kwenye daladala aliyoikamata............
Moshi. Ofisa wa polisi mwenye cheo cha
Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani
Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa
amelikamata.Hata hivyo, haikujulikana… Read More
Basi lingine lapata ajali, laua 18..................
WATU 18 wamekufa papo hapo wakiwemo
askari Polisi wanne katika ajali ya barabarani, wakati basi
linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipoparamia watu hao wakati
wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugon… Read More
Jaji Warioba awalipua wanaomsaliti Mwl.Nyerere.................
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wanasiasa wanaomtuhumu
kwa kumsaliti Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhusu Muungano,
ndiyo wasaliti kwa kuwa waliingiza kw… Read More
Diwani wa CCM kata ya Igalula,Tabora afariki dunia..........
Diwani Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Igalula wilayani Uyui mkoa wa
Tabora, Seleman Kapalu amefariki dunia kwa maradhi ya kifua. Taratibu za
Mazishi zinaendelea.MUNGU AMLAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.…… Read More
0 comments:
Post a Comment