Facebook

Tuesday, 6 May 2014

Mapigano makali yaanza tena Sudan Kusini.....



Mapigano makali yamekuwa yakiendelea katika mji wa Bentiu nchini Sudan Kusini ambapo vikosi vya serikali vinajaribu kuurejesha mji huo uliotekwa na waasi.
Mwandishi wa Habari  aliyeandamana na kikosi cha Umoja wa Mataifa nje ya mji huo anasema amesikia milio ya bunduki na silaha nzito nzito ambapo pia ameona kikosi cha majeshi ya serikali kikijipanga.
Hata hivyo amesema bado haijajulikana ni kundi gani kwa sasa linaloshikilia mji huo wa wenye utajiri wa mafuta.
Kwa upande serikali nchini Sudan kusini inasema majeshi yake yameudhibiti mji wa huo na ngome ya waasi ya Nasir.
Baadhi ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliokimbia makazi yao hivi karibuni kutokana na vita
Mjumbe wa Umoja wa mataifa mjini humo anasema mji huo umedhibitiwa upya na kikosi cha serikali katika operesheni kubwa iliyoanza hapo jana Jumapili.
Shambulio hilo linajiri siku mbili baada ya rais Salva Kiir kumwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo ya amani ya moja kwa moja na kiongozi wa waasi, Riek Machar.

Related Posts:

  • Watu zaidi ya 50 wauawa Uganda.   Watu wasiopungua 50 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia vituo vya polisi na kambi za jeshi nchini Uganda, kwa mujibu wa jeshi. Miongoni mwa waliokufa ni washambuliaji 41 na polisi pamoja na raia 17… Read More
  • Marekani yachukizwa na hatua ya Israel Ghasia kati ya Palestina na Israel Marekani imesema kuwa ina wasiwasi mwingi kwamba maafisa wa Polisi wa Israel wamempiga vibaya kijana mmoja raia wa Marekani. Idara ya maswala ya kigeni imesema kuwa inashtumu utumij… Read More
  • Watu 20 wauawa katika mashambulio mawili katika Pwani ya Kenya.   Watu wasiopungua 20 wameuawa katika mashambulio mawili katika kaunti mbili kwenye pwani ya Kenya usiku wa kuamkia Jumapili. Watu walioshuhudia matukio hayo wamesema, watu wenye silaha nzito walishambulia eneo … Read More
  • Vita kali yazuka Yemen. Ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa kumekuwa na vita vikali kati ya jeshi la taifa hilo na waasi wa ki-shia kazkazini mwa taifa hilo kufu… Read More
  • 29 wauawa katika shambulizi, kenya Wizara ya maswala ya ndani nchini Kenya inasema kuwa takriban watu thelathini wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika makaazi ya pwani ya ke… Read More

0 comments:

Post a Comment