Rais Enrique Pena Nieto wa Mexico anayepunga mkono
Afisa mmoja mwandamizi wa Umoja
wa Mataifa amesema Mexico imekua ikiwatesa watuhumiwa inaowashikilia
katika maeneo mbali mbali ya taasisi za serikali kuanzia jeshi,
serikalini hadi jeshi la polisi.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mateso,
Juan Mendez amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakiteswa wakati wa
kukamatwa na hata wakati wa wakupelekwa mahakamani mbele ya majaji.
Wanajeshi wa Mexico
Aidha Afisa huyo ameongezea kuwa mabadiliko katika sekta ya sheria kama vile kuwapatia mawakili wafungwa, kutapunguza mateso hayo.
Rais Enrique Pena Nieto amelipa kipau mbele swala hilo la kupunguza mateso hayo na kusema kuwa atatekeleza mapendekezo hayo.
0 comments:
Post a Comment