Mshindi mara mbili wa medali ya
dhahabu na raiya wa Uingereza Mo Farah amesema kuwa atashiriki michezo
ya Jumuiya ya madola mwaka huu mjini Glasgow.
“ Nataka kuwajulisha kuwa nitashiriki riadha
katika michezo ya Jumuiya ya Madola. Tuonane Glasgow,” aliandika kwenye
mtandao wa Twitter.Farah mwenye umri wa miaka 31 alimaliza wa nane katika mbio za masafa marefu zilizofanyika mwezi Aprili mjini London na kuchukua muda kuamua iwapo atarejea katika mbio za Glasgow au la.
Kocha wake Alberto Salazar alikuwa amemshauri asishiriki tena mbio za masafa marefu hadi baada ya michezo ya Olimpiki mwaka 2016 itakayofanyika mjini Rio, Brazil.
Tangazo hilo ni habari njema kwa watayarishi wa michezo, huku bingwa wa olimpiki wa mchezo wa 'Heptathlon' akikosa kushiriki baada ya kujifungua. Bingwa wa mbio fupi Usain Bolt pia hajasema iwapo atashiriki
Alisema mda mfupi tu baada ya mbio hizo kuwa alitaka kushiriki vitengo zaidi vya mbio, ingawa alimaliza dakika nne nyuma Wilson Kipsang katika mbio za masafa marefu za London.
Kadhalika anatarajiwa kushiriki mbio za kitengo spesheli cha Diamond League, huku michezo ya Jumuiya ya madola ikitarajiwa kuanza siku 11 baadaye.
Iwapo Farah atashiriki mbio za mita 5000 Jumapili tarehe 27 na mita 10000 au mita 1500 Ijumaa tarehe 1 kunategemea uamuzi wake.
Farah alimaliza wa 9 katika mbio za mita 5000 mwaka wa 2009 wakati wa michezo ya Commonwealth ya Melbourne lakini akajiondia katika mbio hizo mwaka wa 2010 kwa sababu ya uchovu.
Jaribio lake la kukimbia zaidi ya maili 26.2 limesababisha uvumi kwamba huenda akashiriki mbio za mita 10,000 na vitengo viwili vingine vya mbio katika michezo ya Olimpiki ya Rio.
0 comments:
Post a Comment