Facebook

Wednesday, 14 May 2014

Njemba lanaswa na denti wa kiume gesti


ISHARA za mwisho wa dunia? Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb amekula kichapo na kuishia mikononi mwa polisi baada ya kunaswa katika nyumba ya kulala wageni (gesti) akiwa na dogo wa kiume aliyedaiwa kuwa ni denti wa sekondari.
Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Zeb akiwa amepigw pingu baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kiume gesti.
Aibu hiyo ya karne ilijiri juzi Jumatatu kwenye gesti hiyo (jina linahifadhiwa) iliyopo maeneo ya Manzese, Dar ambapo jamaa huyo alikutwa chumbani na denti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14.
Kwa mujibu wa chanzo makini , njemba huyo amekuwa na ‘katabia kachafu kakuwafanyia usodoma’ watoto wa kiume.Habari hizo zilidai kuwa ishu hiyo iliwakera wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu ndipo wakaamua kumfungia kazi baada ya kudaiwa kuwa na mtoto huyo chumbani usiku kucha.
Kwa mujibu wa meneja wa gesti hiyo (aligoma kuta jina) ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha kwa chanzo hicho, raia hao walikuwa wakimchunguza njemba huyo kwa muda mrefu kutokana na tabia ya kulala kwenye gesti hiyo na watoto wa kiume.
Njemba aliyekutwa na denti akipanda kwenye difenda.
“Mwanzo tulifikiri anakuja na vijana hao kama marafiki zake wa kawaida lakini tukaingiwa na wasiwasi baada ya kugundua kuwa alikuwa akilala nao kwa kuwabadilisha,” alisema meneja huyo.
Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa chumba kama kawaida.
“Wahudumu waliniambia kuwa jamaa amefika tena na amechukua chumba cha juu lakini safari hii alifika peke yake, ilinishangaza sana kusikia kaja peke yake kwani siyo kawaida yake so sikuamini,” alieleza meneja huyo.
Alidai kwamba asubuhi ya Jumatatu, mishale ya saa 4:00, wahudumu walisikia miguno ndani ya chumba alicholala njemba huyo ndipo wakakifunga kwa nje kisha kuita polisi na vijana  ambao walifika eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’.
Meneja huyo alisema kuwa hafahamu njemba huyo alimuingiza kijana huyo muda gani kwani walimuwekea mtego siku nyingi akawa anachezwa na machale.
Hata hivyo, Jiji la Dar huwa halina dogo kwani wakazi wa eneo hilo walijazana kwenye gesti hiyo kutaka kumpiga jamaa huyo lakini polisi walifanikiwa kuwatorosha eneo hilo na kuwampeleka Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar.
Hadi chanzo hicho kinang’oa nanga kituoni hapo, njemba huyo na kijana aliyekutwa naye walikuwa wakiendelea kuhojiwa


Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua maovu mbalimbali yanayotokea katika jamii ....

0 comments:

Post a Comment