Tuesday, 6 May 2014
Uchunguzi kumbe Makalio Makubwa Kuna Vingi Ndani Yake
Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makalio makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.
Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari.
Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo makubwa ya umetaboli.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba, ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno.
Ingawa suala hilo linaonekama kana kama ni kinyume, lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari. Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi mafuta yanavyochomeka.
Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.
Related Posts:
Mapacha wazaliwa wakiwa wameshikana mikono Mama wa mapcha hawa amesema mapacha wake ni zawadi kubwa kwake Mama mmoja nchini Marekani, amejifungua mapacha waliozaliwa wak… Read More
Uchunguzi kumbe Makalio Makubwa Kuna Vingi Ndani Yake Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate m… Read More
Tahadhari Juu ya Ugonjwa wa Dengue Iwapo itatokea una kila dalili za homa ya dengue, dawa ya kukimbilia kwanza ni Panadol; inashauriwa usimeze KABISA Diclopar wala Diclofenac. Iwapo utameza dawa hizi, utakuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha. Ime… Read More
Mvua ya Samaki yatokea Sri Lanka.... Samaki waliotoka mtoni kutokana na upepo mkali Wakaazi wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufurahishwa na tukio la 'kunyeshewa' na mvua ya Samaki wadogo. Samaki hawa amb… Read More
Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa? Baadhi ya wanawake wanakunywa maji ya Kondo la Nyuma saa chache baada ya kujifungua Hugeuka kuwa uchafu pindi mama anapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya wanawake wana… Read More
0 comments:
Post a Comment