Facebook

Monday, 26 May 2014

Bilionea ashinda uchaguzi wa Ukraine



Matokeo ya kura yaliotangazwa nchini Ukraine yanaonyesha kuwa Tajiri Petro Poroshenko ameshinda awamu ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Poroshenko amepata asilimia 55 huku mpinzani wake wa karibu Yulia Tymoshenko akipata asilimia 13.Bi Tymoshenko amekubali kushindwa.
Huku akitangaza ushindi wake baada ya shughuli ya kuhesabu kura kukamila,Petro Poroshenko amesema kuwa ziara yake ya kwanza baada ya kutawazwa kama rais itakuwa katika eneo la Donbas mashariki mwa taifa hilo ambapo wanaharakati waliojihami wametangaza uhuru wao.
Amesema kuwa atawasemehe watu wanaomiliki silaha,lakini sio wale wanaowauwa raia.
Shughuli ya kuhesabu kura
Tajiri huyo mwenye tajriba ya kisiasa amewahudumia marais kutoka pande zote za kisiasa nchini Ukraine.
Raia wa Ukraine walimpigia kura kwa wingi kwa imani kwamba angeibuka mshindi katika uchaguzi huo.
kulikuwa na ishara kwamba raia nchini humo walikuwa wakitaka kuongozwa na rais mpya haraka iwezekanavyo baada ya miezi sita ya mzozo.
Hata hivyo kiongozi huyo atarithi matatizo mengi.
Poroshenko anataka Ukraine kujiunga na Ulaya lakini anajua anahitaji kujenga uhusiano na Urusi huku uchumi wa taifa hilo ukiendelea kuzorota.

0 comments:

Post a Comment