Facebook

Monday, 26 May 2014

Cristiano Ronaldo 'Akopy' na 'kupest' staili ya Mario Balotelli

Cristiano Ronaldo (kushoto) akishangilia bao lake la penalti dhidi ya Atletico Madrid. Kulia ni Mario Balotelli alipofunga bao katika nusu fainali ya Euro 2012 kati ya Italia na Ujerumani.
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ‘amekopi na kupesti’ staili ya mshambuliaji wa AC Milan Mario Balotelli baada ya kufunga bao la nne dhidi ya Atletico Madrid kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo.
Cristiano Ronaldo baada ya kufunga bao la nne dhidi ya Atletico Madrid.
Ronaldo baada ya kufunga bao hilo kwa penalti, alishangilia kwa kuvua jezi na kisha kutunisha misuli kama alivyofanya Balotelli alipofunga bao katika nusu fainali ya Euro 2012 kati ya timu yake ya Taifa Italia na Ujerumani.
Baada ya tukio hilo, Ronaldo alionyeshwa kadi ya njano japo hakuonekana kujali. Kwenye fainali hiyo, Real Madrid walishinda kwa bao 4-1 na kutwaa kombe.
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali za michezo kwa wakati na muda muafaka

Related Posts:

  • Simba SC 1-0 Ruvu Shooting FULL TIMEKIKOSI CHA SIMBA IVO MAPUNDA MOHAMED HUSSEIN WILLIAM LUCIAN RAJABU ISIHAKA OWINO MKUDE RAMADHANI SINGANO SAID NDEMLA TAMBWE AWADH JUMA OKWI KIKOSI CHA RUVU SHOOTING ABDALLAH MADEGA MGUTA MSESE NTEBE DABI KEYALA NADI MATHAYO M… Read More
  • Simba Sc Vs Ruvu shooting Live Commentaries KIKOSI CHA SIMBA IVO MAPUNDA MOHAMED HUSSEIN WILLIAM LUCIAN RAJABU ISIHAKA OWINO MKUDE RAMADHANI SINGANO SAID NDEMLA TAMBWE AWADH JUMA OKWI KIKOSI CHA RUVU SHOOTING ABDALLAH MADEGA MGUTA MSESE NTEBE DABI KEYALA NADI MATHAYO… Read More
  • Swansea waigaragaza Arsenal Ligi kuu Uingereza. Klabu ya Swansea November 9 2014 imeendeleza ubabe mbele ya vilabu vikubwa vya ligi kuu ya Uingereza ambapo wakicheza kwenye uwanja wao wa Liberty, Swansea ambao waliwafunga 2-1 Man United kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi hi… Read More
  • Chelsea yaisambaratisha Liverpool .   Kwa mara nyingine Chelsea imeonyesha ni moto wa kuotea mbali baada ya kuifunga Liverpool 2 - 1 mbele ya mashabiki wao katika uwanja wa Anfield. Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lililotiwa wavuni na … Read More
  • BantuTz LIVESTREAMING::SWANSEA CITY vs ARSENALAngalia MechiLiveStreaming kupitia Computer au Tablet yako mechi kali kati ya Swansea dhidi ya Arsenal itakayochezwa majira ya saa 1:00 kwa masaa ya Afrika Mashariki. Utaangalia mechi hiyo bila kukwama au kukatika kwa matanga… Read More

0 comments:

Post a Comment