Tuesday, 6 May 2014
Kinana Amtaka Maalim Seif Ajiuzulu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad, kama kweli hataki Muungano wa serikali mbili, amuandikie barua Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein na kujiuzulu wadhifa wake wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja.
Kinana alisema anachokifanya Seif ni sawa na kuwaramba vichogo wanasiasa wenzake wa upinzani, wakati yeye akipata mshahara na marupurupu mengine, yanayomwendeshea maisha yake chini ya serikali ya CCM.
Alisema kama kweli Maalim Seif anajigamba ni jasiri, achukue uamuzi sahihi wa kujiuzulu wadhifa wake, ili apate nafasi ya kutosha kuwatumikia wananchi nje ya Serikali.
Kinana alieleza kuwa kutembea nchi nzima kwa Seif, si kitendo cha uungwana kufanywa na kiongozi mwenye wadhifa wa Makamu wa Kwanza wa Rais, akiwa ndani ya Serikali inayomlipa mshahara na huduma nyingine muhimu, akaamua kuwachochea wenzake, ambao wako nje ya Serikali kuleta chokochoko dhidi ya Serikali anayoitumikia.
Maalim Seif ameshatuhumiwa kuwa kigeugeu katika maisha yake ya kisiasa, ambapo hivi karibuni Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mohammed Seif Khatib, alielezea namna kiongozi huyo wa CUF, alivyowahi kuwa mtetezi wa serikali mbili alipokuwa kiongozi katika Serikali ya CCM, ambako alitumia nguvu kubwa kupinga vuguvugu la kudai serikali tatu mwaka 1984.
Related Posts:
Kakobe "Nyerere sio Mungu naye alikuwa na mapungufu yake"..."Tanganyika huru lazima ipatikane".........fuatilia hapa kauli mbalimbali za kakobe......... Amesema Tanganyika huru lazima ipatikane ni suala la muda tu Nchi yetu imekuwa katika laana kwa muda mrefu kwa sababu tumeshindwa kuilinda mipaka yetu Moto wa kudai Tanganyika umewaka na hamna mtu awezaye k… Read More
Maaskofu watoa msimamo wao kuhusu katiba..............fuatilia hapa.................... Katika salama za pasaka viongozi wa dini wa katoliki 32 wamesema maoni ya wananchi katika rasimu ndio msingi wa katiba hivyo wamewataka wajumbe wa bunge la katiba wa yaheshimu kama yalivyo wasilishwa na jaji wario… Read More
Waisalamu na Maaskofu waungana kutetea rasimu ya Warioba.......................fuatilia hapa............ Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania imeungana na maaskofu mbalimbali kuwataka wajumbe wa Bunge la Katiba kuheshimu Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa kwa mujibu wa sheria na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Pia, … Read More
Maige apinga serikali tatu,adai itakuwa maajabu ya dunia .......................fuatilia hapa............. Mjumbe wa Bunge la Katiba, Almas Maige amesema endapo wajumbe wa Bunge hilo watapitisha muundo wa Serikali tatu, nchi itaingia katika kitabu cha maajabu ya dunia cha Guiness Book of Records. “Hili litakuwa shirik… Read More
Ili kunusuru bunge,Sitta aifuta UKAWA Zanzibar.........soma hapa.......... Wakati viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiweka kambi Zanzibar, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana naye alitumia siku nzima visiwani humo akikutana na baadhi ya viongozi wa… Read More
0 comments:
Post a Comment