Tuesday, 6 May 2014
Mrisho Ngasa" Azam Wametushika Pabaya"
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa amesikia taarifa za kuondoka kwa Didier Kavumbagu na Frank Domayo akatamka: “Aisee hilo ni pigo kubwa kwa kikosi chetu naomba niwe muwazi.”
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Mwanza anakouguza majeraha ya nyama za paja, Ngassa alisema amepokea taarifa za kuondoka kwa Kavumbagu na Domayo kwa masikitiko na kuongeza wachezaji hao walikuwa wakihitajika katika kikosi chao.
Ngassa alisema maumivu zaidi yanakuja kutokana na ukweli kwamba wachezaji wote walikuwa katika kikosi cha kwanza cha Yanga, ambapo sasa uongozi unatakiwa kutuliza akili kutafuta mbadala wa nyota hao walioondoka wakiwa wachezaji huru baada ya kumaliza mikataba.
“Tuseme kweli kwamba kuondoka kwa Didier na Domayo ni pengo kwa timu, hili lipo wazi kwani walikuwa wachezaji muhimu katika timu yetu, walicheza mechi nyingi ambazo ni muhimu, ni wakati wa viongozi kufanya kazi yao ipasavyo kuhakikisha wanatafuta wachezaji wengine mahiri ili kuziba nafasi zao,”alisema Ngassa ambaye amewahi kucheza Azam na Simba
Related Posts:
Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya. Kiungo wa Sunderland Adam Johnson huenda akajiunga na AS Monaco ya Ufaransa 9Sun), Sergio Aguero amesisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka Manchester City (Daily Star), Rafael Benitez… Read More
Manchester United wako katika hatua za mwisho kumsajili staa wa Athletico Bilbao Ander Herrera. Manchester United iko katika hatua za mwisho kumsajili mchezaji wa Kihispaniola Ander Herrera anayekipiga katika klabu ya Athletico Bilbao ambaye anatarawa kusiani mkataba wa miaka minne kwa dau la uhamisho la Paundi m… Read More
Thomas Vermaelen atua Manchester United ! Kuna taarifa nzito kuwa Thomas Vermaelen wa Arsenal anakaribia kusaini Manchester United. Inasemekana atahama kutoka Arsenal kwende Manchester United kwa ada ya uhamisho ambayo haijafahamika huku akitarajia ku… Read More
Antonio Valencia aongezwa mkataba Man Utd Antonio Valencia amekuwa mchezaji wa kwanza kusainishwa mkataba mpya na kocha Louis van Gaal kwa muda wa miaka 3.… Read More
Diego Costa:Najiunga na Chelsea Diego Costa amesema kwamba anajiunga na Chelsea kwa sababu 'ni moja ya klabu kubwa kabisa duniani'. Straika huyo wa Atletico Madrid kwa muda mrefu sasa amekua akitarajiwa k… Read More
0 comments:
Post a Comment