Facebook

Monday, 26 May 2014

Kocha wa Atletico ajitetea baada kufungwa



Kocha Mkuu wa Atletico Madrid Diego Simeone amekiri kuwa alifanya makosa kumpanga Diego Costa katika mechi ya fainali baina ya timu hiyo na Real Madrid.
Real Madrid hapo jana iliibamiza Atletico Madrid kwa jumla ya magoli 4 - 1 na kunyakua kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya.
Costa alibadilishwa baada ya kuumia msuli wa paja ikiwa ni dakika 9 mechi hiyo imeanza
Mshambuliaji huyo raia wa Hispania aliumia alipocheza mechi baina ya Atletico na Barcelona wiki moja iliyopita na ameweza kuifungia magoli 36 timu katika msimu huu.
"Hakuna mashaka kiwango alichoonyesha Diego uwanjani nina wajibu wangu nilifanya makosa lazima nikubali," Kocha Simeone alisema.
Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Brazil alionekana kuwa chini ya kiwango na alibadilishwa na Adrian Lopez.
"Sitaki kupoteza muda tulicheza pungufu mchezaji mmoja", Kocha huyo alisema.

Related Posts:

  • Siagi ya Uruguay yanaswa Brazil Siagi ya Uruguay ilinaswa na maafisa wa uwanja wa ndege Brazil Wasimamizi wa uwanja wa ndege Brazil wamezuia takriban kilo 39 za siagi ya… Read More
  • Yaya na Kolo Toure wafiwa na mdogo wao, Ibrahim Nyota wa Ivory Coast Yaya na Kolo Toure wametaarifiwa kuhusu kifo cha mdogo wao wakati wakiwa kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil. Ibrahim Toure alifariki siku ya Alhamisi mjini Manchester, akiwa na umri wa … Read More
  • Uingereza 1- 2 Uruguay Suarez ashangilia bao lake dhidi ya Uingereza Uruguay wameilaza Uingereza 2-1 katika mechi yao ya pili ya kundi D. Luiz Suarez ndiye amefunga mabao yote mawili ya Uruguay Uingereza walikuw… Read More
  • FIFA kuchunguza Mexico kwa ubaguzi Shirikisho la kandanda Duniani FIFA limeanza kuchunguza hatua ya kuiadhibu Mexico, baada ya madai kujitokeza kuwa mashabiki wake walihusika katika ma… Read More
  • Uingereza yaondolewa Brazil Uingereza imebanduliwa nje ya kombe la dunia Brazil. Uingereza wameondolewa kutoka kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil baada ya raundi ya kwanza, k… Read More

0 comments:

Post a Comment