Facebook

Tuesday, 13 May 2014

Masharti ya Boko Haram kuhusu wasichana


Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekahu
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
Wakati huohuo Waziri wa mambo ya ndani nchini Nigeria amesema serikali haitakubali masharti ya kundi la Boko Haram kwamba kwanza liwaachilie wapiganaji wake kabla ya wasichana zaidi ya miambili waliotekwa nyara waachiliwe.
Waziri Abba Moro amsema ni jambo la kipuuzi sana kwa kundi la kigaidi kujaribu kuweka masharti kama hayo.
Mwandishi mjini Maiduguri John Simpson anasema kuwa masharti yaliyotolea na kundi hilo ni ishara kuwa liko tayari kufikia makubaliano na serikali
Wasichana watatu kati ya waliooyeshwa na kuongea katika kanda hiyo walikuwa wanavalia hijabu. Mmoja alisema kuwa amesilimu wakati mwingine akisema yeye tayari ni Muisilamu

0 comments:

Post a Comment