Beki wa Liverpool na Ivory Coast Kolo Toure amepata malaria, na kushindwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Bosnia-Herzegovina.
Toure aliugua wakati akisafiri kwenda Marekani, lakini anatazamiwa kuwa atapona na kuwa tayari kabla ya Kombe la Dunia kuanza.
"Hakushiriki mchezo dhidi ya Bosnia lakini atarejea mapema wiki ijayo," amesema mkuu wa madaktari wa timu, profesa Cyrille Dah.
Yaya Toure pia aliukosa mchezo huo kutokana na tatizo la misuli.
Ivory Coast wapo kundi C pamoja na Columbia, Ugiriki na Japan.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali za kimichezo na burudani
0 comments:
Post a Comment