Mtoto huyo ambaye ni kipa, Jose amekuwa akiichezea timu ya Fulham ya watoto chini ya umri wa miaka 14, lakini alikuwa hawezi kujiunga na timu hiyo rasmi hadi hapo Fifa ilipotoa ruhusa.
Chini ya sheria za Fifa, klabu zinapaswa kutoa ushahidi wa kutosha kwenye usajili wa mtoto kwamba jambo hilo halihusiani na soka na badala yake kutoa mkataba kama mwanafunzi.
Mtoto huyo wa Mourinho mwanzoni alikuwa akichezea timu ya watoto ya Real Madrid, Canillas wakati baba yake alipokuwa kocha Santiago Bernabeu kabla ya kuhamia England mwaka jana.
Jose alivutia sana kwenye majaribio yake ya wiki tano Fulham mwanzoni mwa msimu, lakini hakusaini mkataba hadi hapo Fifa mwezi uliopita ilipotoa ruhusa kwa mtoto kusainishwa na timu hiyo kama mwanafunzi.
0 comments:
Post a Comment