Mlinzi kiraka wa timu ya Young Africans Mbuyu Junior Twite leo ameongeza
mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga baada
ya kufikia makubaliano na uongozi na kupata majibu ya Shirikisho la Soka
nchini TFF juu ya idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa msimu ujao
2014/2015.
Usajili wa Twite umefanyika leo makao makuu ya klabu ya Yanga chini ya
Katibu Mkuu Bw Beno Njovu ambapo mchezaji amesema ataendelea kujitolea
kwa uwezo wake kuisaidia timu yake ya Yanga.
Katibu Mkuu wa Young Africans Beno Njovu amesema wameingia mkataba wa
mwaka mmoja na Twite baada ya pande zote kukubaliana, hivyo kuanzia sasa
Twite ataendelea kuwa mchezaji wetu kwa msimu ujao wa 2014/2015 na
kusisitiza kuwa usajili ndio umeanza sasa.
Akiongea mara baada ya kuweka sahihi kwenye mkataba wake mpya Twite
amesema anajisikia furaha kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga, kwani
anafurahia maisha ya Jangwani, wapenzi, washabiki, viongozi na wachezaji
ni marafiki/ndugu ndani na nje ya Uwanja.
Aidha Twite amesema Yanga ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika,
zenye washabiki na waachama wengi hivyo wangu ni fahari kuendelea
kuitumika timu hii ambayo tangu kujiunga nayo nimekua nikijtoa kwa moyo
wangu wote kusaka mafanikio.
Mbuyu Twite amekua ni mchezaji wa Young Africans kwa kipindi cha miaka
miwili tangu Julai 2012 alposajiliwa huku katika kipindi hicho chote
akiwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliweza
kuisadia timu yake kutwaa Ubingwa wa Lig Kuu ya Vodacom na msimu huu
kushika nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment