Wednesday, 14 May 2014
Tottenham Hotspurs yamtimua kocha wake ‘Tim Sherwood’
Kibarua cha kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Tim Sherwood kimeota nyasi baada ya klabu hio kutangaza kufukuzwa kazi kwa kocha huyo. Hii ni baada ya miezi 6 kwenye kazi hio na kuonekana hafai kumiliki game za klabu hio pale White Hart Lane.
Fahamu Sherwood alirithi nafasi hio kutoka kwa kocha Andre Villas-Boas mwezi wa 12 mwaka jana na kupewa mkataba wa mwaka na miezi sita. Mwazi wa Nne palikuwa na tetesi kuwa kocha huyu atafukuzwa baada ya msimu kuisha. Bosi wa Spurs Daniel Levy ana mpango wa kutafuta kocha bora wa kuendeleza klabu hio.
Rekodi
-Akiwa Spurs Sherwood ameshinda game 14 katika game 28 alizosimamia.
-Spurs imemaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi msimu huu. nafasi ya 6 katika msimamo.
-Tim ameshapata kazi klabu nyingine ya Brighton baada ya kujiuzulu kwa kocha Oscar Garcia .
Endelea kutembela katemimethsela.blogspot.com uweze kupata habari mbalimbali za michezo
0 comments:
Post a Comment