Algeria ambayo ilikuwa
imeshindwa 2-1 na Ubeljiji katika mechi yao ya ufunguzi katika kundi H
iliingia katika mechi hii ikifahamu fika endapo itashindwa basi
haitakuwa na budi kuweka tayari mipango ya kurejea nyumbani.
Algeria hata hivyo ilijifurukuta na kuilaza Korea Kusini mabao 4 - 2 katika uwaja wa Porto Alegre.Dakika mbili baadaye Rafick Halliche alifunga bao la pili kwa kichwa kabla ya Abdelmoumene Djabou kufunga bao la tatu kunako dakika ya 38 ya a kipindi cha kwanza .
Hata hivyo utepetevu wa wa safu ya ulinzi ya the Desert Foxes uliiruhusu japana kufunga bao la kufutia machozi dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza .
Mfungaji alikuwa ni Song Heung-min.
Vijana wa Vahid Halilhodzic walijikakamua na kufunga bao la nne kupitia kwa Yacine Brahimi kunako dakika ya 62 ya kipindi cha pili.
Kulikuwa na nyakati ambapo Algeria ilikuwa imelemewa kwa kasi na mfumo wa mchezo lakini walibahatika na kustahimili mashambulizi ya Korea .
Ushindi huo ulikuwa wa kihistoria kwao kwani ulikuwa nio ushindi wa Kwanza tangu mwaka wa 1982.
Aidha hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa timu kutoka Afrika kufunga mabao manne katika kombe la dunia.
Kinachosubiriwa sasa ni kuona mabadiliko yatakayofanyika katika timu hiyo ya Vahid Halilhodzic kabla ya mechi yao ya mwisho dhidi ya Urusi. Algeria wanaweza fuzu kwa mkondo wa 16 bora iwapo wataishinda Urusi
Ubeljiji wamekwisha fuzu kwa mkondo wa pili baada ya kuibana Urusi katika mechi ya awali.
Algeria sasa ni ya pili katika kundi hilo ikiwa na alama 3 . Urusi na Korea Kusini zinaalama moja kila moja.
0 comments:
Post a Comment