Facebook

Thursday, 26 June 2014

Ander Herrera asajiliwa rasmi Manchester United !

        Mabingwa wa zamani wa England Manchester United Leo hii wametangaza kuwa Kiungo kutoka Spain Ander Herrera amesainiwa Klabuni hapo kutoka klabu ya Athletic Bilbao.
Herrera, mwenye Miaka 24, amesaini Mkataba wa Miaka Minne kukiwa na Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka mmoja zaidi.
Kiungo huyo, ambae sasa anasubiri Shahada ya Kimataifa ya Uhamisho ili kuubariki kikamilifu Uhamisho huu, alijiunga na Bilbao Mwaka 2011 akitokea Real Zaragoza na kuichezea Mechi 128 na kufunga Bao 11.
 Photo: Amesaini mkataba wa miaka minne, huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba mwengine pindi unapoisha au unapokaribia kuisha.. Karibu jembe!! 

=/ D.P /=
           Pia amezichezea Timu za Taifa za Vijana za Spain za chini ya Miaka 20, U-20, na pia U-21 na U-23.
Mchezaji huyo anakuwa wa kwanza kusainiwa chini ya Meneja mpya Louis van Gaal ambae sasa yuko huko Brazil kama Kocha wa Netherlands.
       Akimpokea Mchezaji huyo mpya, Meneja Msaidizi wa Man United, Ryan Giggs, alisema: “Ander ni Kijana mdogo hodari mwenye nguvu na ubunifu. Tunaamini yeye ni Chipukizi atakaeng’ara sana huko Spain na nina hakika atapendwa na Mashabiki wetu. Nimefurahi ameichagua Manchester United. Nangojea kwa hamu tuwe nae kwenye Ziara ya kabla Msimu mpya huko Marekani.”
     Nae Ander Herrera amesema: “Kusaini Manchester United ni ndoto iliyotimia. Nimecheza Old Trafford na Athletic Club kwa Mechi za Ulaya na hiyo ni kumbukumbu kubwa kwangu. Nimejiunga ili kuisaidia Klabu kutimiza malengo yake yote. Ninafuraha sasa kuishi Jijini Manchester na nangojea kwa hamu nivae Jezi Nyekundu inayosifika ya United. Sitasahau muda wangu na Athletic Club na nataka niwashkuru Mashabiki wote na Wafanyakazi kwa sapoti yao na juu ya yote nawashkuru Wachezaji wenzangu wa zamani na kuwatakia kila la heri hapo baadae.”
TAKWIMU zinazoonesha viungo waliopo Manchester United na kiungo mpya aliyetambulishwa. Hizi ni kwa msimu uliopita 2013/2014.

IDADI YA MECHI.
Ander Herrera - 33
Michael Carrick - 29
Tom Cleverley - 22
Marouene Fellain - 16
Darren Fletcher - 12

IDADI YA PASI WALIZOPIGA
Ander Herrera - 1523
Michael Carrick - 1997
Tom Cleverley - 1107
Marouene Fellain - 794
Darren Fletcher - 657

NAFASI ZA MAGOLI
Ander Herrera - 53
Michael Carrick - 28
Tom Cleverley - 10
Marouene Fellain - 5
Darren Fletcher - 7

UKABAJI/ KUCHUKUA/KUNYANGANYA MIPIRA
Ander Herrera - 75
Michael Carrick - 43
Tom Cleverley - 40
Marouene Fellain - 31
Darren Fletcher - 6

IDADI YA MASHUTI WALIYOPIGA
Ander Herrera - 68
Michael Carrick - 17
Tom Cleverley - 15
Marouene Fellain - 25
Darren Fletcher - 5

MAGOLI WALIYOFUNGA
Ander Herrera - 5
Michael Carrick - 1
Tom Cleverley - 1
Marouene Fellain - 0
Darren Fletcher - 0

MAGOLI WALIYOTENGENEZA
Ander Herrera - 5
Michael Carrick - 0
Tom Cleverley - 0
Marouene Fellain - 1
Darren Fletcher - 0

MAFANIKIO UWANJANI
Ander Herrera - 38
Michael Carrick - 6
Tom Cleverley - 5
Marouene Fellain - 9
Darren Fletcher - 3

Ander Herrera amewazidi viungo wote wa Manchester United katika idara zote. Ni idara 1 tu ya kupiga pasi ambapo kiwastani Michael Carrick anakuwaga bora takribani miaka 6 mfululizo iliyopita

SOURCE:SKY SPORT
             manutd.com

Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment