Facebook

Tuesday, 24 June 2014

Manchester United wako katika hatua za mwisho kumsajili staa wa Athletico Bilbao Ander Herrera.

 
Manchester United iko katika hatua za mwisho kumsajili mchezaji wa Kihispaniola Ander Herrera anayekipiga katika klabu ya Athletico Bilbao ambaye anatarawa kusiani mkataba wa miaka minne kwa dau la uhamisho la Paundi million 28 linaloweza kufikia hadi Paundi million 30 na atakuwa analipwa mshahara wa £145,000 kwa wiki.

   Kinachosubiriwa ni makubaliano binafsi kati ya wawakilishi na wanasheria wa Man Utd na mchezaji mwenyewe kisha kufanyiwa vipimo vya afya.

   United wanataka kufanikisha dili hilo mapema zaidi kabla ya mwezi June ambapo dau la kumpata Kiungo huyo litafikia Paundi million 32.Kwa taarifa zilizoripotiwa ni kwamba dili hilo linaweza kukamilika kabla ya Jumatano.

Ander Herrera (r) faces Barcelona's Alexis Sanchez    Manchester United kipindi hiki wanaonekana wako makini zaidi kwani katika dirisha la usajili la majira ya joto United walionekana kutokuwa makini zaidi kwani ilikuwa inasemekana watu 3 waliaonekana katika makao makuu ya Chama cha soka cha Uhispania lakini United walikuwa hawana taarifa na watu hao na dili likashindikana.

  Louis Van Gaal yuko katika hatua za awali kabisa kukiimarisha na kukisuka upya kikosi cha Manchester United kwani tayari imesharipotiwa beki wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya soka ya  Southampton Luke Shaw yuko mbioni kujiunga na klabu hiyo mara baada ya michuano ya kombe dunia.

  Ander Herrera ambaye aalikuwa miongoni wa wachezaji walioshiriki katika michuano ya Olympic mwaka 2012 akiwa na timu ya taifa ya Hispania na vilevile alikuwa ni nguzo muhimu katika kikosi cha Athletico Bilbao msimu ulioisha na kuisaidia klabu yake kushika nafasi ya nne,atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Man United.
  Ander Herrera ni zao la shule ya soka ya Athletico Bilbao lakini baadaye aliibukia katika klabu ya Real Soceadad na kurudi tena Bilbao.

SOURCE: SKY SPORTS
              BBC FOOTBALL

Imeandaliwa na.....
                              < Katemi Methsela>


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment