Facebook

Monday, 23 June 2014

Origi aisaidia Ubeligiji kusonga mbele


  Kinda aliyezaliwa Kenya na kuchukua uraiya wa Ubeligiji Divock Origi alifungia Ubeligiji bao la pekee na la ushindi dhidi ya Urusi katika mechi yao ya pili ya kundi H.
Bao hilo la dakika za mejeruhi za mechi hiyo ndiyo iliyoiwezesha Ubeljiji kufuzu kwa mkondo wa pili wa timu kumi na sita bora.
Origi ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku alifuma bao hilo la kipekee kunako dakika ya 88 ya kipindi cha pili ya mechi hiyo alipopokea pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard .
Ubelgiji ilikuwa tayari imeilaza Algeria mabao 2-1 katika mechi ya kwanza .
Awali Ubeljiji ilikuwa imemjaribu Igor Akinfeev ila mkwaju wake Kevin Mirallas ukagonga mwamba.
Ushindi huo uliiwacha Ubeljiji kileleni mwa kundi hilo wakiwa na alama 6 baada ya ushindi wao wa pili.
Wenyeji wa mashindano yajayo ya kombe la dunia mwaka 2018 Urusi watalazimika kufanya kazi ya ziada ilikufuzu kufuatia matokeo mawili ya kwanza huko Brazil
Lukaku; Ubeljiji 1-0 Urusi
Urusi ilikuwa imetoka sare na Korea katika mechi yao ya kwanza.
Hata hivyo Kocha Fabio Capello amesalia na mechi dhidi ya Algeria kujaribu bahati yake na mfumo mpya kabla ya kuabiri ndege ya Moscow.
Nchini Kenya ambapo Origi alikuza kipaji chake ,wakenya wamemmiminia sifa kedekede kinda huyo ambaye babake aliwahi kuichezea Harambee Stars .
Evelyn Wambui ‏kwenye tweeter alisema kuwa #Origi anaiwakilisha kenya katika kombe la dunia #TeamKenya in the #Worldcup2014 !
@kevojuice naye aliandika kuwa Origi ndiye mchezaji wa kwanza wa kenya kucheza kwenye kombe la dunia '' 1st Kenyan to score in World Cup...!!! #Origi hehe...

Related Posts:

  • FIFA kuchunguza Mexico kwa ubaguzi Shirikisho la kandanda Duniani FIFA limeanza kuchunguza hatua ya kuiadhibu Mexico, baada ya madai kujitokeza kuwa mashabiki wake walihusika katika ma… Read More
  • Siagi ya Uruguay yanaswa Brazil Siagi ya Uruguay ilinaswa na maafisa wa uwanja wa ndege Brazil Wasimamizi wa uwanja wa ndege Brazil wamezuia takriban kilo 39 za siagi ya… Read More
  • Uholanzi yasonga mbele, Brazil Uholanzi ni timu ya kwanza kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia. Uholanzi ilitoka mabao 2-1, nyuma na kuishinda Australia mabao 3-… Read More
  • Uingereza 1- 2 Uruguay Suarez ashangilia bao lake dhidi ya Uingereza Uruguay wameilaza Uingereza 2-1 katika mechi yao ya pili ya kundi D. Luiz Suarez ndiye amefunga mabao yote mawili ya Uruguay Uingereza walikuw… Read More
  • Okocha amlaumu kocha wa Nigeria. Nahodha wa zamani wa Nigeria Jay Jay Okocha amemlaumu kocha Stephen Keshi kwa timu yake kushindwa kucheza vizuri katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia kundi F dhidi ya Iran siku ya Jumatatu. Timu hizo zilitok… Read More

0 comments:

Post a Comment