Baada ya tetesi zilizodumu kwa muda mrefu kuhusu Carlos Vela kurejea Arsenal, The Gunners wameamua kuuza shea zao zilizobakia zinazohusu usajili klabuni Real Sociedad.
Arsenal wamepokea £8.8m kwa ajili ya kuondoa kipengele cha kumnunua tena Vela kwa bei kiduchu na wanaweza kupewa tena hadi £4m kutegemea na idadi ya michezo atakayoichezea klabu hiyo ya Spain.
Kwa sasa iwapo Arsenal itamuhitaji Vela basi ada haitakua tena £3.5m bali ni ile watakayoitaka Real Sociadad. Na iwapo atauzwa kwa timu nyingine kuna asilimia chache watapewa Arsenal.
Umeliaonaje hilo dili?
0 comments:
Post a Comment