Facebook

Sunday 22 June 2014

Picha ya mhalifu yawavutia Wanawake, Wapanga Kuchangisha Pesa Kumtoa Jela

Kitengo cha polisi cha Stockton, California kimezua mjadala mpya baada ya kupost kwenye Facebook picha za mhalifu ili kipate msaada wa taarifa zaidi za raia lakini kilichotokea na kuwa picha hiyo imewavutia zaidi wanawake walibaki kuzungumzia uzuri wa mwanaume huyo.

Picha ya mhalifu huyo aliyetajwa kwa jina la Jeremy Meeks (30) anayekabiliwa na kiesi ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria imepata likes zaidi ya 66,000 na comments zaidi ya 20,000 kutokana na uzuri wa mhalifu huyo.


Jeremy anatakiwa kutoa kiasi cha $900,000 ili aachiwe huru. Lakini wanawake wengi waliocomment kwenye picha hiyo wanazungumzia kuhusu kuchangia pesa ili wamtolee dhamana.

0 comments:

Post a Comment