Ureno ambayo ilikuwa na
matumaini ya kushinda, ilienda sare ya 2-2 na Marekani na kuepuka
fedheha ya kufungashwa virago katika hatua ya makundi katika kombe la
dunia linaloendelea huko Brazil.
Kwa upande wao Marekani, ilikuwa inafahamu fika
kuwa matokeo baina ya 2-2 naina ya Black Stars ya Ghana na vinara wa
kundi G Ujerumani ilikuwa na hatari ya kuinyima fursa ya kushiriki
mkondo wa pili wa kombe la dunia kwa hivyo ilikuwa inatafuta ushindi
ambao ingeipa tiketi ya moja kwa moja katika hatua ijayo.Vijana wa Jurgen Klinsmann ndiyo walionekana na tamaa zaidi ya kushiriki mkondo wa pili wa kombe la dunia walipofaidi kona iliyotokana na makosa ya Ricardo Costa
na wakaitumia vyema.
Marekani ilifufua matumaini ya kusonga mbele Clint Dempsey alipovurumisha mkwaju ndani ya neti na kuiweka timu yake mbele , hata hivyo Christiano Ronaldo alimwandalia pasi nzuri na akaisawazishia Ureno katika muda wa ziada wa mechi hiyo.
Marekani inahitaji ushindi mkubwa dhidi ya Ujerumani ambayo itakuwa ikitafuta sare ya aina yeyote ilikusonga mbele.
Ghana kwa upande wao sasa wanahitaji kuichapa Ureno na kuomba kuwa Ujerumani nayo itaitandika Marekani iliwafuzu kwa mkondo ujao.
Kufikia sasa ujerumai inaongoza kundi hili ikiwa na jumla ya ponti 4 sawa na Marekani.Ghana ni ya 3 na alama 1 sawa na Ureno .
0 comments:
Post a Comment