Facebook

Monday, 30 June 2014

Joel Camplee apata kibali cha kucheza Uingereza,aleta ahueni kwa Arsenal.

JOEL CAMPBELL APATA KIBALI CHA KAZI ENGLAND
Photo: JOEL CAMPBELL APATA KIBALI CHA KAZI ENGLAND 

Joel Campbell amethibitisha kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba amepokea kibali cha kufanya kazi nchini England jana.

Mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Arsenal misimu miwili iliyopita kutoka klabu yake ya nyumabani ya Saprissa, amekua akicheza kwa mkopo nje ya England sababu kubwa ikiwa ni kunyimwa kibali cha kufanya kazi England. 

Campbell alisema: “Nina furaha nimepokea kibali cha kazi nchini England…Bado nasubiri mambo mazuri,” alitweet.

Baada ya kufanya makubwa na kucheza mechi za kutosha timu ya taifa ya nchi yake(Costa Rica) ili kufaulu kupata viza na kubali cha kazi, sasa kijana huyo mwenye miaka 21 anaweza kushiriki katika michezo  ya maandalizi msimu mpya na the Gunners. 

Ingawa anaonekana anaweza kuwemo katika kikosi cha jumla cha Arsenal, lakini ni mapema kusema kama Campbell ataweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza Emirates msimu mpya ujao. 
Kwani kwa sasa inasememkana Wenger yupo mbioni kusajili straika ili kuongeza ushindani kwa Lukas Podolski, Olivier Giroud na Yaya Sanogo. 
Ila kwa sasa ni rahisi kusema kwamba ataweza kucheza klabu za Premier League kwa mkopo hasa Crystal Palace wameshaanza kuonesha kumtaka kwa mkopo kwa ajili ya msimu ujao. 

Maoni Yako

0 comments:

Post a Comment