Facebook

Friday, 27 June 2014

Lallana anafanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na Liverpool


         Adam Lallana yuko jijini Liverpool akifanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na "The Reds".Ikumbukwe Southampton walikataa dau lililotolewa na Liverpool mara mbili kabla ya michuano ya kombe la dunia.Lakini safari hii mchezaji mwenyewe ameonyesha nia ya kuondoka na tayari Southampton wamemfungulia milango ya kuondoka na kujiunga na majogoo wa jiji la Liverpool kwa dau la uhamisho la Paundi million 25.
         Anafuata nyayo za aliyekuwa  mchezaji mwenzake wa Southampton,Rickie Lambert ambaye alijiunga na Liverpool kabla ya michuano ya Kombe la dunia.
          Inaonekana ni biashara nzuri wanayoifanya Southampton ya kuuza wachezaji wao kwa bei ya juu sana kinachosubiriwa na mashabiki wa Southampton ni kuona wachezaji gani wapya watakaonunuliwa kuja kuziba nafasi zilizoachwa na Adama Lallan na Rickie Lambert waliojiunga na Liverpool na vilevile Luke Shaw aliyejiunga na Manchester United.

Imeandaliwa na......
                                ~Katemi Methsela

SORCES:SKY SPORTS
            BBC SPORTS


Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa na tetesi zote za usajili wa wachezaji barani Ulaya.Jukumu letu ni kukuhabarisha punde tunapopata hhabari yoyote kwa muda na wakati muafaka.

0 comments:

Post a Comment