Uingereza inakabiliwa na
upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za
matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.
Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.
Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.
Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.
Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.
0 comments:
Post a Comment