Facebook

Tuesday, 24 June 2014

Mwanafunzi Ujerumani anasa katika sanamu ya nyeti za kike

Haijatajwa endapo hilo ni tukio la kwanza au yashawahi kuwakuta watundu wengine.
Haijatajwa endapo hilo ni tukio la kwanza au yashawahi kuwakuta watundu wengine.
Mwanafunzi mmoja nchini Ujerumani alilazimika kuokolewa baada ya kunasa katika sanamu ya nyeti za kike zilizoundwa kwa jiwe.

Inaaminika mwanafunzi huko kutoka Marekani aliingia ndani ya sanamu hiyo kwenye mji wa Tubingen. Hata hivyo baada ya kuingia alinasa na kutoka ikawa mbinde.
Ililazimu gari tano za huduma ya dharura na wazima moto 22 kumnasua kijana ambaye jina lake halijafahamika baada ya kunasa kwenye sanamu ya nyeti za kike.
Kijana huyo, ambaye miguu yake ilikwama ndani na chini ya sanamu hii iliyowekwa kwa lengo la sanaa, alionekana kudhalilika baada ya kunasuliwa.
Erick Guzman, aliyepiga picha hizo na kuzichapisha mtandaoni, alisema: ‘Nilikuwepo pale!!! Lengo lake lilikuwa kupiga picha ya kuchekesha.
‘Waokoaji hawakufurahishwa na tukio hilo, na yeye mwenyewe alionekana kudhalilika.’
Sanamu hiyo ilijengwa na msanii ajulikanaye kwa jina la Fernando de la jara  kutoka Peru na imekuwepo katika chuo kikuu cha Tubingen nchini Ujerumani kwa zaidi ya miaka 13 kwenye kitengo cha Microbiology.
Sanamu hiyo inaitwa Pi-Chacan, ambayo ina maana ya kufanya mapenzi katika lugha ya kihindi cha Peru.

0 comments:

Post a Comment