Mwanamume mmoja katika jimbo la
Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili
baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini NIGERIA.Duru katika hospitali hiyo zimesema kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa kwa matatizo ya kiakili na kwamba hataendelea kuzuilikwa kwa muda mrefu.
Jimbo la Kano lina idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu, na limekuwa chini ya sheria za kiisilamu tangu mwaka 2000.
Licha ya kufahamishwa kuwa mwanamume huyo hana tatizo lolote la kiakili, familia ya Bala ilitafuta ushauri wa daktari mwingine aliyewafahamisha kuwa hatua yake ya kumkana Mungu, inatokana na matatizo ya kiakili.
Bwana Bala, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu, alilazimishwa kupata ushauri wa daktari wa kiakili , ingawa alitumia simu kuwasiliana na wanaharakati wa haki za kibinadamu.
Hospitali ambako alikuwa ana pokea matibabu ilisema katika taarifa yake kuwa Bwana Bala hana tatizo lolote la kiakili na kuwa yuko sawa.
Alilazwa hospitalini kwa sababu alihitaji kuchunguwa na daktari, ilisema taarifa ya hospitali hiyo
0 comments:
Post a Comment