Brazil imeponea kung'olewa kutoka mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini humo.
Hii ni baada ya mechi ya kwanza ya mkondo wa
mtoano kati yake na Chile kumalizika kwa mikwaju ya Penalti baada ya
timu hizo mbili kwenda sare ya bao moja baada ya kipindi kizima cha
mechi.Wakati wa mikwaju ya Penalti, Brazil ilishinda tatu huku Chile ikishinda mbili.
Wakati wa mechi , Brazil ilifunga bao la kwanza la mechi ndani ya kipindi cha kwanza, lakini Chile ilileta jibu kabla ya kipindi cha kwanza cha mechi kukamilika.
Brazil ilikuwa na kibarua kigumu na shinikizo tele kutoka kwa mashabiki wa Brazil ambao walijaa uwanjani na pia kwa kuwa Brazil ni mwenyeji wa michuano hiyo ,matarajio ya wengi nchini Brazil ni kuwa wanatafanya vyema katika mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment