Facebook

Saturday, 28 June 2014

Barcelona inataka kumsajili Suarez licha ya adhabu kali aliyopewa.


Licha ya kukabiliwa na marufuku ya FIFA ya miezi minne kwa kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Barcelona ya Uhispania haijakata tamaa ya kumsajili mshambulizi machachari wa wa Uruguay Luiz Suarez.
Mshambulizi huyo wa kutegemewa wa klabu ya Liverpool ya Uingereza amepigwa marufuku ya miezi minne kumaanisha kuwa hatoshiriki mechi yeyote hadi mwezi Oktoba.
Aidha Suarez hatoweza hata kufanya mazoezi katika kipindi hicho.
Haijulikani kwanini mabingwa hao wa zamani wa kombe la mabingwa barani uropa ambao wanajivunia huduma za Lionel Messi wa Argentina na Neymarwa Brazil bado wanamtaka Suarez.

Liverpool ilimnunua Suarez kwa pauni milioni £25m mwezi Januari 2011 kutoka klabu ya Ajax.
Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.

0 comments:

Post a Comment