Facebook

Monday 30 June 2014

Mfalme wa Saudi Arabia awashukia Waislamu wenye misimamo mikali

ISIL ni kundi la kijihadi lenye nguvu ambalo limeshiklilia eneo kubwa nchini Iraq, lengo lao ni kutaka kuanzisha serikali ya Kiislamu nchini humo.
ISIL (Islamic State of Iraq and Levant) ni kundi la kijihadi lenye nguvu ambalo limeshiklilia eneo kubwa nchini Iraq, lengo lao ni kutaka kuanzisha serikali ya Kiislamu nchini humo.
Siku ya Jumapili, Mfalme wa Saudi Arabia, Abdullah aliwakosoa vikali waislamu wenye misimamo mikali, “akiwakemea magaidi waache kuwatisha Waislamu”, kwenye hotuba yake ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhan.
Uislamu ni “dini ya umoja, mshikamano na ya kusidiana”, ila kuna baadhi ya watu “wamerubuniwa na miito ya uongo, inayowafanya kuufanya Uislamu uwe ni ugaidi”, alisema kiongozi huyo wa kifalme.
“Lengo lao ni kuleta utengano miongoni mwa Waislamu”, alisema huku akitolea mfano wa ghasia zinazofanywa na Islamic State of Iraq and the Levant (ISIL).
Kundi la kijihadi lenye nguvu ambalo limekuwa likiongoza kwa ghasia zinazofanywa na Wasunni nchini Iraq tangu June 9, walivyoweza kushika hatamu ya miji ya kaskazini na kushikilia maeneo makubwa.
ISIL hufanya shughuli zao Syria na Iraq na lengo ni kuanzisha serikali ya Kiislamu katikati ya mpaka wa mataifa hayo mawili, ila hali nchini Iraq inazitishia nchi za Jordan na Saudi Arabia.
“Hatutaruhusu magaidi, kuutumia Uislamu kwa malengo yao binafsi, kuwatisha Waislamu au kuzidunisha nchi na watu wake”, alisema Abdullah.
Mfalme huyo wa Saudia pia aliwatakia Waislamu wote “ulinzi, mafanikio na uimara” kwenye kipindi hiki cha Ramadhan ambao kwa nchi nyingi umeanza siku ya Jumapili.
Wakati wa Ramadhan, ambao ni mwezi mtukufu kwa Waislamu kwa sababu ni mwezi ambao kiutamaduni Koran ilishushwa mwezi huo kwa Mtume Muhammad (S.A.W), waumini wanakatazwa kula, kunywa, kuvuta, na kufanya ngono kuanzia mawio mpaka machweo.

0 comments:

Post a Comment