Facebook

Sunday, 29 June 2014

‘Wamatumbi’ wagoma kuondoka Ujerumani

Maombi ya hifadhi ya wakimbuizi hao wa muda mrefu yamekataliwa na serikali ya Ujerumani.
Maombi ya hifadhi ya wakimbizi hao wa muda mrefu yamekataliwa na serikali ya Ujerumani.
Mamia ya maafisa wa polisi wameizunguka shule ya zamani mjini Berlin ambayo imekaliwa na wakimbizi wa muda mrefu ambao hawataki kuondoka.
Wakimbizi hao wa Afrika wanataka haki ya kubaki Ujerumani, pamoja na kukataliwa kwa maombi yao ya hifadhi.
Adam, mkimbizi kutoka Sudan ambaye alitaja jina moja tu, aliwaambia waandishi wa habari kwamba siku ya Ijumaa wakimbizi hao walipanda kwenye dari ya shule hiyo na walikuwa tayari kuruka kama polisi hao wangeingia ndani.
Mgomo huo ulihusisha wakimbizi 40-80 huku wakiwa na wafuasi ndani ya jengo hilo baada ya polisi kuingia humo mapema wiki hii na kuwafurusha wakimbizi 200 ambao walikuwa humo tangu 2012.
Maafisa wa mji wanasema watajadiliana na wakimbizi hao kuhusu mahitaji endapo wataondoka kwenye jengo hilo.
Hao jamaa hawatupendi, basi tu, wamesahau kuwa ndio waliosababisha tukafikia hali hiyo…(1884/85)

0 comments:

Post a Comment