Facebook

Saturday 28 June 2014

Uingereza yaomba ruhusa ya jeshi lake

Wanajeshi wa Uingereza
Uingereza imesema kuwa inafanya mazungumzo na kenya ili kutatua mzozo kuhusu mafunzo ya wanajeshi wa Uingereza nchini humo.
Serikali ya Kenya inaaminika kuchelewa kuwaruhusu wanajeshi zaidi wa Uingereza kuingia nchini humo ili kufanya mazoezi.
Maelfu ya wanajeshi wa Uingereza huzuru nchini kenya kila mwaka kwa mafunzo ya wiki sita lakini hilo limesitishwa kwa mda baada ya kenya kuchelewa kutoa ruhusa ya kidiplomasia kwa ndege inayowabeba wanajeshi wanaotarajiwa kufanya mafunzo hayo.
Hatua hiyo inaonekana kama kulipiza kisasi kwa tahadhari ya kusafiri humu nchini iliotolewa na serikali ya Uingereza kwa raia wake ambayo imeathiri pakubwa sekta ya utalii nchini.
Wanajeshi wa Uingereza wamekuwa wakifanya mafunzo nchini kwa zaidi ya miongo minne lakini makubaliano kati ya mataifa hayo mawili kuhusu mafunzi hayo yanakamilika mwezi Aprili.
Masineta kutoka upande wa chama tawala nchini kenya wamemtaka rais Uhuru kenyatta kutotia sahihi mkataba mpya.
Maafisa katika ubalozi wa Uingereza wameiambia BBC kwamba wana matumaini mgogoro huo utatatuliwa kwa haraka.
Wizara ya maswala ya kigeni nchini kenya hatahivyo inasema kuwa swala hilo tayari limetatuliwa.

0 comments:

Post a Comment