Wachezaji wa kikosi cha timu ya
taifa ya Ghana Sulley Muntari na Kevin Prince Boateng wamefukuzwa katika
timu hiyo kwa ukosefu wa nidhamu.
Taarifa kutoka mtandao wa shirikisho la soka nchini humo imesema kuwa wawili hao wametimuliwa mara moja.Naye mchezaji wa AC Milan Sulley Muntari ameadhibiwa kwa kumshambulia afisa mmoja wa kamati kuu ya timu hiyo
Shirikisho la soka nchini Ghana limeongezea kwamba kisa kinachomuhusu Muntari kilitokea siku ya jumanne na kumtaja Moses Armah,mwanachama wa usimamizi wa timu hiyo kama mtu aliyeshambuliwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.
Wakati huohuo Boateng amedaiwa kutojali matamshi aliyoyatoa.Habari hizo zinajiri siku moja baada ya serikali ya Ghana kutuma dola millioni 3 nchini Brazil ili kuwalipa wachezaji wa timu hiyo nchini Brazil fedha zao za kushiriki katika michuano ya kombe la dunia.
Timu hiyo inayojulikana kama Black Stars ilikuwa imetishia kususia mechi kati yake na Ureno iwapo haitapewa fedha hizo swala lililoilazimu serikali kuingilia kati.
0 comments:
Post a Comment