Kocha wa Uruguay Oscar Tabarez
amesema kuwa atajiuzulu kama mwakilishi wa FIFA katika kamati mbili
tofauti za kiufundi kupinga adhabu kali iliyotolewa na shirikisho hilo
dhidi ya nyota wa Uruguay Luiz Suarez.
Tabarez anasema kuwa adhabu hiyo kali
iliyotolewa ya marufuku ya miezi minne dhidi yake ilikuwa kisingizio tu
FIFA inanjama dhidi ya Uruaguay .Tabarez, alidai kuwa FIFA ilitoa adhabu hiyo kufuatia ushawishi wa vyombo vya habari haswa za kizungu .
Suarez alimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani wa dunia 1-0 jumanne iliyopita.
FIFA imeamuru asishiriki mechi yeyote ile kwa kipindi cha miezi minne mbali na kulipa faini ya pauni 65000. (£65,680).
Awali katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke alimtaka Suarez atafute matibabu ya kisaikolojia wakati akitumikia marufuku hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.
0 comments:
Post a Comment