Kocha wa Uholanzi Louis van
Gaal anatarajia shirikisho la soka duniani FIFA litawaruhusu wachezaji
wake kunywa maji katika mechi yao ya raundi ya pili dhidi ya Mexico
itakayochezwa katika uwanja wa Castelao ulioko katika eneo la
Fortaleza.
Fortaleza ni eneo linaloshuhudia viwango vya juu vya nyuzi joto.Ni dhahiri kuwa mwili wa binadamu yeyote unastahili maji kwa hivyo hawa wachezaji naamini kuwa wanastahili kunywa maji ilikuzuia wasishikwe na kisunzi .
Kiungo wao Leroy Fer, ambaye anauguza jeraha la goti anasema kuwa Uholanzi ilipata kionjo tu cha kucheza katika hali ya kiwango cha juu mno cha joto baada ya kuwasili huko wakitoka Rio de Janeiro.
Fer anasema kuwa japo Uholanzi imezoea kucheza katika maeneo ya Uropa yenye baridi kali,Uholanzi itajikaza kisabuni kwani ni hali ileile itakayoikumba timu pinzani ya Mexico.
0 comments:
Post a Comment