Mtangazaji maarufu Salim Kikeke wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC
ametwaa taji la Mtangazaji wa Runinga Anayependwa katika toleo la kwanza
la Tuzo za Watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards katika sherehe zilizofanyika Serena Hotel, Ijumaa jijini Dar Es Salaam.
Vipengele 11 (kumi na kimoja) vilikuwa vikishindaniwa. Mshindi katika
kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na
tuzo. Chini ya orodha ni picha za tukio hilo.
ORODHA YA WASHINDI
1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
Millard Ayo – Clouds FM
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
Amplifaya – Clouds FM
3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
Salim Kikeke – BBC Swahili
4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
Mkasi – EATV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
Juma Kaseja – Yanga
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
Nisher
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
My Number One – Diamond
8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
Yahaya – Lady Jaydee
09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
King Majuto
10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
11. FILAMU INAYOPENDWA
Ndoa Yangu
Salim
Kikeke wa BBC Dira ya Dunia, mshindi wa kipengele cha Mtangazaji wa
Runinga Anayependwa, akizungumza machache baada ya kutangazwa.
Mkongwe
King Majuto akiwapa mashabiki wake heko kwa kumpigia kura. Ameshinda
kipengele cha Muigizaji wa Kiume Anayependwa Kwenye Filamu. Pembeni ni
Lulu Michael, mshindi wa Mwigizaji wa Kike Kwenye Filamu Anayependwa.
Picha ya pamoja ya walionufaika katika Tuzo za Watu mjini Dar Es Salaam, Juni 27, 2014.
Hamza Kasongo, mkongwe katika fani ya utangazaji Tanzania akimkabidhi Tuzo Salim Kikeke.
Luca Neghesti na Nancy Sumari waandaaji wa shughuli ya Tuzo za Watu. Wao pia wanahusika na Bongo5.com.
Salim Kikeke (katikati), Mtangazaji wa Runinga Anayependwa akiwa na Luca Neghesti na Nancy Sumari waandalizi wa Tuzo za Watu.
MC Jimmy Kabwe akiwa kazini – Tuzo za Watu 2014.
Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lynn
Faraja Nyalandu
Salim Kikeke wa BBC, Mzee wa Dira ya Dunia TV.
Jacqueline Wolper naye alikuwepo.
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
Kichwa
chenyewe ndiyo hiki, Luca Neghesti mwasisi wa Tuzo za Watu. Kijana ana
mipango mizuri, anastahili kuungwa mkono. Boss wa Bongo5 pia.
Millard Ayo wa Clouds FM akifika kuchukua tuzo yake.
Mutu ya Kilo, JB
JB akimkabidhi Lulu Michael tuzo ya Mwigizaji wa Filamu wa Kike Anayependwa.
Sasa
hapa Majuto (kofia nyeupe) huwezi kujua anaigiza au la! Lakini huyu
kweli mkongwe, toka enzi za DDC Magomeni Kondoa, chuma kimedumu sana
hiki. Jacqueline Wolper yuko na simu, sijui ni Instagram au…!?
Washindi wa Tuzo za Watu.
Kwa warembo hawa, hapa King Majuto lazima kaongezeka umri.
Millard Ayo wa Clouds FM,yuko smart sawa sawa,yeye kaondoka na mtangazaji wa redio anayependwa.
Imeandaliwa na........
Katemi Methsela
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment