Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amekataa kutaja wachezaji wake watakaofunga mwezi wa Ramadhani, kabla ya mchezo wao wa Jumatatu (leo) dhidi ya Ujerumani.
Katika mkutano na waandishi wa habari, alikasirishwa baada ya kuulizwa suala hilo mara kadhaa.
"Hili ni suala binafsi, na kuuliza ni kukosa heshima na maadili" alisema kocha huyo kutoka Bosnia.
"Wachezaji watafanya wanavyotaka, na sitaki mtafaruku huu uendelee." Ameongeza.
Nahodha wa Algeria Madjid Bougherra amesema atafunga Ramadhani, lakini kiungo wa Ujerumani Mesut Ozil na beki wa Ufaransa Bacary Sagna walisema hawatofunga.
Kikosi cha Algeria kimekwenda Brazil na Hakim Chalabi, ambaye ni mtaalam wa utabibu wa michezo na mmoja wa wataalam wa kutegemewa wa FIFA kwa wachezaji wanaofunga Ramadhani.
0 comments:
Post a Comment