STRAIKA
wa Uruguay Luis Suarez amefungiwa Miezi Minne kutoshiriki chochote
kwenye Soka baada ya kupatikana hatia ya kumuuma Meno Beki wa Italy
Giorgio Chiellini.
Straika huyo wa Liverpool pia amefungiwa Mechi 9 za Kimataifa zitakazomfanya awe nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Adhabu hii pia inamaanisha atazikosa Mechi 9 za kwanza za Klabu yake Liverpool za Ligi Kuu England kwa Msimu mpya.
Tukio hili la kumng’ata Meno Chiellini
lilitokea Juzi Jumanne kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi D la Fainali za
Kombe la Dunia ambayo Uruguay iliifunga Italy 1-0 na kutinga Raundi ya
FIFA imetamka haitazungumza lolote
kuhusu Kesi ya Luis Suarez anaetuhumiwa kumng’’ata Meno Beki wa Italy
Giorgio Chiellini hadi Kamati ya Nidhamu imalize shauri lake lakini
Wadau na Malejendari wa Klabu ya Liverpool wamezungumza kwamba Mchezaji
huyo ameiaibisha na kuifedhehesha Klabu yake hiyo.
Suarez alionekana akimng’ata Meno
Chiellini kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia
ambayo Nchi yake Uruguay iliifunga Italy Bao 1-0 na kutinga Raundi ya
Pili ya Mtoano.
Refa Marco Rodriguez wa Mexico, ambae
huko kwao amebatizwa Jina ‘Dracula’ kwa ukali wake Uwanjani, hakuona
tukio hilo na licha ya Chiellini kumwonyesha alama za Meno hakuchukua
hatua yeyote.
Hata hivyo Kanuni za FIFA zinaruhusu
Mchezaji kuhukumiwa kwa ushahidi wa Video hata kama Refa aliliona tukio
na kutochukua hatua.
Suarez amepewa hadi Usiku wa Leo Saa 5
Usiku, Saa za Bongo, kujibu tuhuma hizo ambazo akipatikana na hatia FIFA
inao uwezo wa kumfungia Mechi 24 au Miaka miwili kote Duniani kwa Mechi
za Ndani, za Klabu, na za Kimataifa.
Akizungumzia Shauri hilo, Msemaji wa
FIFA Bibi Delia Fischer amesema: “Uchunguzi unaendelea na bado ni
mapema. Hatuwezi kuzungumza nini kitatokea hilo lipo mikononi mwa Kamati
ya Nidhamu. Tutatoa tamko baadae Leo au Kesho mara tu wakiamua.”
Kifungo cha juu kabisa kumkumba Mchezaji
kwa kosa wakati wa Fainali za Kombe la Dunia ni kile cha Mwaka 1994 kwa
Mchezaji wa Italy, Mauro Tassotti, cha Mechi 8 baada kumvunja Pua kwa
kiwiko Mchezaji wa Spain, Luis Enrique, ambae sasa ni Meneja mpya wa
Barcelona.
Wakati huo huo, Malejendari wa
Liverpool, Phil Thompson na Robbie Fowler, wamezungumzia tukio la hivi
sasa la Luis Suarez na kudai Mchezaji huyo ameiaibisha na kuifedhehesha
Klabu yake Liverpool.
Phil Thompson, Nahodha wa zamani na
Meneja Msaidizi wa Liverpool, amesema: “Nilivunjika nguvu kabisa
nilipoona picha zile na kutaka hilo lisingetokea tena. Huyu ni Mchezaji
Bora wa England, anaichezea Klabu yangu na ameleta aibu, ameleta fedheha
klabuni!”
Nae Mchezaji wa zamani wa Liverpool, Robbie Fowler, amesema Suarez ameipaka matope Liverpool.
Hii si mara ya kwanza kwa Suarez
kung’ata Meno Mpirani kwani Aprili 2013, Luis Suarez alifungiwa Mechi 10
kwa kumuuma Meno Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic kwenye Mechi ya
Ligi Kuu England.
Mwaka 2010 huko Uholanzi, Suarez alifungiwa Mechi 7 kwa kumuuma Kiungo wa PSV Eindhoven Otman Bakkal.
Wachambuzi wengi huko England wanahisi
tukio hili litamng’oa Liverpool na kutokomea huko Spain kujiunga na Real
Madrid au Barcelona kama mwenyewe alivyokuwa akitaka tangu Msimu
uliopita.
0 comments:
Post a Comment