Uholanzi ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
Mabao ya Uholanzi yaliyofungwa na Leroy Fern na
Memphis Depay yaliyowapa ushindi dhidi ya Chile katika mechi ngumu
iliyochezewa jijini Sao Paulo.Mechi hiyo ilikosa msisimko na kuishia sufuri bin suifuri kufikia muda wa mapumziko ,Lakini Fer alifunga kwa kichwa katika dakika ya 77, kabla ya Depay kufunga katika dakika ya mwisho.
Huenda Chile wakachuana na Brazil katika mechi za muondoano, huku upande wa Luiz Van Gaal ukitarajia kuchuana na aidha Mexico au Croatia.
Uholanzi ilikuwa bila mshambulizi Robin Van Persie ambaye alikuwa anatumikia marufuku baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.
Mshambulizi wa Barcelona Alexis Sanchez alionekana kutaka kufunga bao la kwanza kwa Chile kwa weledi wake na pasi ambazo ziliwahangaisha mabeki wa Uholanzi kwa muda.
Arjen Robben alikuwa karibu kuendeleza rekodi yake ya kufunga bao katika kila mechi baada ya mkwaju wake kukosa lango.
Ilikuwa hadi dakika ya 65 wakati mlindalango Jasper Cillessen alipolazimika kuokoa mkwaju wa Sanchez uliopigiwa karibu na lango.
Hilo liliwatia waholanzi motisha na kumfanya Robben kupiga mkwaju uliomlenga Claudio Bravo katika lango la Chile baada ya kuwapiga chenga mabeki kabla ya Depay kuokoa kutoka kwa mlindalango kwa kuondoa katika maeneo ya hatari.
Kufutia ushindi huo Uholanzi wanatuchana na mshindi wa pili katika kundi A yaani Mexico.
Huku Chile ikiratbiwa kuvaana na mshindi wa kundi A yaani Brazil katika mechi za maondoano .
0 comments:
Post a Comment